arrow-small-left Created with Sketch. arrow-small-right Created with Sketch. Carat Left arrow Created with Sketch. check Created with Sketch. circle carat down circle-down Created with Sketch. circle-up Created with Sketch. clock Created with Sketch. difficulty Created with Sketch. download Created with Sketch. email email Created with Sketch. facebook logo-facebook Created with Sketch. logo-instagram Created with Sketch. logo-linkedin Created with Sketch. linkround Created with Sketch. minus plus preptime Created with Sketch. print Created with Sketch. Created with Sketch. logo-soundcloud Created with Sketch. twitter logo-twitter Created with Sketch. logo-youtube Created with Sketch.

Vulval and vaginal health (Swahili) - Afya ya vulva na ya uke

Ni muhimu kutunza vulva yako na uke wako (sehemu ya siri ya kike). Hali nyingi ambazo zinaathiri eneo hili ni kawaida na ni rahisi kutibu. Lakini ni muhimu kuzungumza na daktari wako ikiwa una wasiwasi.

Kuna tofauti gani na vulva yako na uke wako?

Watu wengine wanafikiri vulva na uke ni kitu kimoja - lakini ni tofauti. Vulva yako ni sehemu ya nje ya sehemu ya siri ya kike ambayo inaonekana. Inajumuisha:

 • sehemu inayokuwa na mavuzi (nyewele ya mbeleni)
 • midomo ya nje, ambayo imekuwa na nywele za sehemu ya siri (labia majora)
 • midomo ya ndani, ambayo haikuwa na mavuzi (labia minora)
 • kisimi na kifuniko chake
 • ufunguzi wa mkojo (ambapo mkojo unatoka)
 • ufunguzi wa uke.

Uke wako uko ndani mwili wako. Uke unaenea kutoka vulva yako kwenda kwa mwanzo wa mfuko wa uzazi. Uke wako upo ambapo hedhi yako hutiririka kutoka kwa mfuko wa uzazi, ambapo unaweza kupenya (k.m. ngono) na ambapo watoto hupitia wakati wa kuzaliwa.

Mchoro wa vulva na uke

Mchoro unaoonyesha sehemu tofauti ya uke.

Nini inaweza kuathiri eneo hili?

Mwasho

Ngozi ya uke wako ni dhaifu sana, kwa hivyo vitu vingi vinaweza kusababisha kuwasha.

Mwasho wa uke unaweza kusumbua. Dalili zinaweza kujumuisha:

 • kuchoma au kujikuna
 • hisia ya msisimko chini ya ngozi yako
 • rangi ya nyekundu au uvimbe
 • ufa au mpasuko wa ngozi
 • ngozi ziwe nyeupe
 • ngono yenye maumivu.

Utoko

Wanawake wote wana utoko wa uke na majimaji ambayo yanaweka uke na uke unyevu na afya. Lakini wakati mwingine utoko unasababishwa na maambukizi.

Maambukizi

Kuna maambukizi mbalimbali yanayoweza kuathirika vulva na uke, kwa mfano, ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani (thrush). Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (thrush), unaosababishwa na Kandida, unaoathiri karibu 75% ya wanawake angalau mara moja katika maisha yao.

Maambukizi ya uke yanaweza kusababisha dalili kama vile:

 • mchomo au mwasho karibu na ukeni
 • utoko wa uke ambao una harafu au rangi tofauti kuliko ya kawaida
 • hisia ya uchungu wakati wa kujisaidia
 • uvimbe au rangi ya nyekundu wa vulva na uke
 • mipasuko ya ngozi ya vulva (uke)
 • ngono yenye maumivu.

Mzio na hali za ngozi

Baadhi ya bidhaa zinaweza kusababisha mwitiko wa mzio ambao ungeweza kuwasha vulva (uke) iwe rangi ya nyekundu. Kwa mfano, visodo (tampons), sabuni, suruali inayobana ya usanisi (Lycra) na klorini (kutoka mabwawa ya kuogelea). Kuna hali nyingine za ngozi zinazoweza kuathiri vulva (uke).

Kuzeeka

Wakati wa kukoma hedhi, ngozi zako za uke zinaweza kuwa nyembamba zaidi, kusababisha ukavu, mwasho na maumivu wakati wa ngono.

Maumivu ya uke

Maumivu ya uke yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali. Kwa mfano, maambukizi, hali za ngozi, kubana kwa misuli ya sakafu ya nyonga, uharibifu wa neva na uharibifu wa tishu kutokana na upasuaji au kujifungua.

Wakati wa kumwona daktari wako

Ni muhimu kumwona daktari wako ikiwa una wasiwasi kuhusu muwasho, utoko au maumivu ya uke.

Daktari wako huenda kufanya mtihani, uchunguzi au vipimo vingine ili kujua ni nini inayosababisha tatizo. Kulingana na sababu, anaweza kukupa marashi, krimu au vidonge. Aanaweza pia kutoa ushauri juu ya jinsi ya kutunza eneo hili. Katika baadhi ya visa, anaweza kukurejelea kwa mtaalamu.

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kutunza uke wako kwa kusoma kijitabu cha Jean Hailes 'The vulva’ (kupatikana katika Kiingereza pekee).

Ili kupata maelezo, nyenzo na marejeleo, tembelea kwa jeanhailes.org.au/health-a-z/vulva-vagina.