arrow-small-left Created with Sketch. arrow-small-right Created with Sketch. Carat Left arrow Created with Sketch. check Created with Sketch. circle carat down circle-down Created with Sketch. circle-up Created with Sketch. clock Created with Sketch. difficulty Created with Sketch. download Created with Sketch. email email Created with Sketch. facebook logo-facebook Created with Sketch. logo-instagram Created with Sketch. logo-linkedin Created with Sketch. linkround Created with Sketch. minus plus preptime Created with Sketch. print Created with Sketch. Created with Sketch. logo-soundcloud Created with Sketch. twitter logo-twitter Created with Sketch. logo-youtube Created with Sketch.

Heavy periods (Swahili) - Hedhi nzito

Hedhi nzito (damu nyingi za hedhi) ni wakati unapopoteza damu nyingi kwa kila hedhi. Takriban mwanamke mmoja kati ya wanne ana hedhi nzito. Jifunza zaidi juu ya hedhi nzito ikiwa ni pamoja na dalili, sababu na chaguzi za matibabu.

Je, unajuaje kama una hedhi nzito?

Inaweza kuwa ngumu kujua kama una hedhi nzito, lakini kuna dalili za kawaida. Kwa mfano:

 • unahitaji kubadilisha vifaa vyako vya hedhi (k.m. pedi, kisodo, kikombe cha hedhi) kila baada ya masaa mawili au chini yake
 • unahitaji kubadilisha vifaa vyako vya hedhi kati ya usiku
 • unatambua mabonge ya damu ambayo ni makubwa kuliko sarafu ya senti 50
 • hedhi yako inadumu zaidi ya siku nane
 • hedhi zako zinakuzuia kufanya mambo unayofanya ya kawaida.

Dalili za hedhi nzito

Ikiwa una hedhi nzito, unaweza:

 • kuwa na mipindano ya misuli au maumivu kwenye tumbo la chini (tumboni)
 • kuonekana kuwa mweupe au unahisi uchovu au kizunguzungu kutokana na kiwango cha chini cha chuma.

Je, ni kitu gani husababisha hedhi nzito?

Hedhi nzito zinaweza kutokana na mabadiliko ya homoni ambayo yanafanya utando wa uterasi wako kukua zaidi kuliko kawaida. Utando huo unatoka na kuwa hedhi. Lakini kunaweza kuwa na sababu nyingine, kwa mfano, endometriosisi, vivimbe, nyuzinyuzi kwenye ukuta wa uzazi au kizazi kuvimba.

Je, hedhi nzito hutambuliwaje?

Ni muhimu kumwona daktari yako ikiwa una wasiwasi kuhusu hedhi nzito na dalili zinaathiri maisha yako ya kila siku. Daktari wako atakuuliza kuhusu historia yako ya matibabu na anaweza kuomba ufanye uchunguzi wa ndani ili kuangalia uterasi na ovari yako.

Anaweza pia kufanya vipimo au chunguzi ili kujua ni nini kinachosababisha tatizo. Kwa mfano, kipimo cha ujauzito, chuma au damu, au skeni ya ultrasound.

Chaguzi za matibabu

Ikiwa unagunduliwa na hedhi nzito, daktari wako atajadiliana chaguzi mbalimbali za matibabu. Kwa mfano:

 • dawa fulani (k.m. dawa za kuzuia uchochezi au asidi ya tranexamic)
 • matibabu ya homoni (k.m. kifaa cha kuingiza uterasi cha Mirena® (kitanzi au IUD) au Kidonge cha kuzuia mimba)
 • projestini (aina za sanisia za homoni ya projesteroni)

Kulingana na sababu ya kutokwa na damu, unaweza kuhitaji kufanyiwa upasuaji. Kwa mfano:

 • hysteroscopy - utaratibu wa siku moja ya kutathmini ndani ya uterasi wako
 • kuyeyusha kwa utando wa uterasi - utaratibu wa siku moja ya kuondoa utando wa uterasi.

Katika hali nyingine, wakati taratibu za kimatibabu au nyingine za upasuaji hazijasaidia kudhibiti kutokwa na damu, huenda ukahitaji kupata upasuaji wa kuondoa uterasi (operesheni isiyoweza kutenduliwa ya kuondoa uterasi na mara nyingi mirija ya uzazi).

Ni muhimu kujadili hatari na manufaa ya kila utaratibu na mtaalamu wako kabla ya kuamua.

Wakati wa kumwona daktari wako

Ikiwa unafikiri una hedhi nzito na dalili zinaathiri maisha yako ya kila siku, umwone daktari wako.

Kwa maelezo zaidi na marejeleo, tembelea ukurasa wa tovuti ya Jean Hailes ya periods-heavy bleeding.